Mwanamuziki wa Bongo fleva, Nuh Mziwanda amekanusha tetesi zilizoenea katika mitandao ya kijamii kuwa yeye na mpenzi wake wa zamani Shilole walikuwa pamoja jijini Mwanza.

Staa huyo amesema kuwa ni kweli alimuona Shilole Mwanza kwenye club ambayo yeye alikuwa anafanya show na aliambiwa kuwa yupo pale lakini hakukutana naye wala ku-kiss na yeye kama ambavyo watu wanadai kuwa waliwaona wakali hao wakiwa pamoja na waki kiss.

Nuhu Mziwanda amesema kuwa “Mimi nimekuja Mwanza kwenye show zangu nimekutana naye tu Club hivyo mimi siwezi kumkataza mtu kuingia sehemu hivyo hilo ni jambo la kawaida, mimi mwenyewe niliambiwa yupo humu so sikujali maana mimi nilienda kufanya kazi na yeye alikwenda kufanya kazi kimpango wake.

Mbali na hilo Nuh Mziwanda anasema kwa yeye saizi ni mume wa mtu hivyo hawezi kufanya mambo ya ajabu ajabu kama hayo kwa kuwa yeye anajiheshimu na kuheshimu ndoa yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *