Baada ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda kuachana na aliyekuwa mke wake, hatimaye msanii huyo amerejea kwenye dini yake ya awali ya ukristo.
Nuh alibadilsha dini kwa ajili ya ndoa na aliyekuwa mke wake wa halali anayefahamika kwa jina la Nawal kabla ya kuvunjika kwa ndoa hiyo.
Taarifa za Nuh kurudi katika dini yake zilienea katika mitandao ya kijamii baada ya kuonekana kanisani Jumapili iliyopita.
Nuh amethibitisha kurudi katika dini yake wakati akifanya mahojiano na kituo maarufu cha radio nchini ambapo ameeleza kuwa ni kweli alikuwa kanisani siku ya Jumapili kama taarifa zilivyozagaa katika mitandao mbalimbali kuwa ameonekana kanisani.
Pia msanii huyo amekanusha taarifa zilizotolewa na aliyekuwa mke wake kuwa ameacha kumjali mtoto wake Anyagile tangu watenganae na kusema tuhuma hizo hazina ukweli.
Pia ameongeza kuwa “Anaongea vibaya kwenye media sio vizuri, mimi na fan base yeye mwanamke anatakiwa ajue anaongea nini, ila muache aongee akikua ataacha.