Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeendelea na kazi ya kuwaondoa wadaiwa sugu katika nyumba za shirika hilo zilizopo maeneo ya Kijichi jijini Dar es Salaam walioshindwa kulipa madeni.

Kaimu meneja mipango na uwekezaji wa shirika hilo, Radhia Tambwe amesema kwamba wadaiwa hao ni wale walionunua nyumba hizo na kushindwa kumalizia deni kwa muda uliopangwa.

Meneja huyo amesema kuwa watu hao wametolewa katika nyumba hizo kwa kufuata taratibu na sheria zilizowekwa na kusisitiza kuwa nyumba hizo zitauzwa tena kwa mara nyingine.

Pia meneja huyo amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu kwa hiyo wasiolipa madeni yao wakamilishe kabla ya shirika hilo alijachukua hatua kali za kisheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *