Mchezaji tenisi namba moja kwa ubora duniani, Novak Djokovic ameshinda taji la kombe la Rogers baada ya kumfunga mjapan, Kei Nishikori kwenye mchezo wa fainali uliofanyika Toronto nchini Marekani.

Mchezaji huyo ambaye ni raia wa Serbia ameshinda jumla ya seti 6-3 7-5 dhidi ya mpinzani wake huyo kutoka nchini Japan.

tennis-grand-slam-novak-djokovic-kei-nishikori_3200888

Nishikori hii ni mara yake ya kwanza kwenye mashindano ya Tenisi tangu apumzike baada ya mashindano ya Wimbledon kutokana na jeraha la ubavu, na amemshinda mpinzani wake seti 7-6 (8-6) ,6-1 kwenye hatua ya pili ya nusu na kutinga fainali hiyo.

Kwa upande wa Djokovic yeye alimfunga Gael Monfils seti 6-3 6-2 hatua ya pili ya nusu fainali huko Toronto na kutinga fainali ambapo ameibuka na ushindi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *