Mchezaji tetesi kutoka Serbia, Novak Djokovic amefungwa na mchezaji namba 117 duniani Denis Istomin raia wa Uzbektan katika michuano ya Australian Open inayoendelea nchini Australia.

Mshindi huyo mara sita wa michuano hiyo amepoteza kwa seti 7-6 5-7 7-6 6-4 kwenye mchezo huo uliokuwa wa kusisimua.

Andy Murray amesalia katika nafasi ya kwanza kushinda tuzo ya Australian open huko mjini Melbourne.

Hii ni mara ya pili pekee katika miaka saba ambapo Djokovic kupoteza ushindi kwa mchezaji aliyeko kati ya wachezaji 100 kushindwa kwake na Juan Martin del Potro aliyekuwa katika nafasi ya 145 katika mashindano ya olimpiki yaliyofanyika huko Rio mwaka 2016.

Denis Istomin atapambana na mhispania Pablo Carreno Busta, aliyemshinda Muingereza Kyle Edmund ifikapo Alhamisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *