Norway kuwa nchi ya kwanza duniani kuzima mawimbi ya radio ya analogia

0
537

Nchi ya Norway imekuwa nchi ya kwanza duniani kuzima mawimbi ya redio ya analogia ambayo yanajumuisha pia masafa ya FM.

Mawimbi hayo yataanza kuzimwa saba na dakika kumi na moja usiku kutokana na makubaliano ndani ya nchi hiyo.

Badala yake, taifa hilo sasa litatumia mawimbi ya dijitali Digital Audio Broadcasting ambayo (DAB).

Mawimbi hayo ya DAB yalianza kuhimarishwa mwaka 1981 na maonesho ya kwanza ya jinsi teknolojia hiyo inafanya kazi yalifanyika Geneva nchini Uswisi mwaka 1985.

Mawimbi ya dijitali huwa na ubora zaidi na hufika mbali yakilinganishwa na ya analogia na gharama yake ni ya chini mno.

Kufikia mwisho wa mwaka huu matangazo yote ya redio za taifa nchini humo yatakuwa yakipeperushwa kwa DAB.

LEAVE A REPLY