Kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Niyonzima leo ameanza mazoezi na timu yake mpya ya Simba aliyojiunga nayo msimu huu.

Niyonzima ambaye amejiunga na klabu hiyo ya Simba akitokea mahasimu wao Yanga kwa mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuichezea klabu hiyo yenye maskani yake maeneo Msimbazi Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Niyonzima amewasili jana jijini Dar es Salaam akitokea kwa Rwanda baada ya mapunziko ya mwisho wa msimu uliopita wakati akichezea klabu ya Simba.

Simba wameanza mazoezi katika uwanja wa Boko Veterani uliopo Ununio jijini Dar es Salaam baada ya kurejea kutokea Afrika Kusini.

Klabu hiyo ipo katika maandalizi ya tamasha la Simba Day linalotarajiwa kufanyika kesho Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mazoezi hayo kikosi hicho kiliwajumuisha wachezaji wake wapya akiwemo Haruna Niyonzima, John Boko, Emmanuel Okwi, Aishi Manula, Said Mohammed na Erasto Nyoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *