Muigizaji nyota wa Bongo movie, Niva amesema kuwa hana tatizo wala bifu na rapa Nay wa Mitego licha ya kutupiana madongo ya maneno miongoni mwao.

Niva amesema kuwa madongo yote waliyokuwa wanatupiana na Nay wa Mitego kwa mwaka 2016 ilikuwa ni ‘bifu’ za kimuziki na mipango ya kibiashara kwa upande wa movie lakini hawana bifu lolote kati yao.

Muigizaji amesema hawajawahi kugombana na wala hawana tatizo lolote na Nay kwa kuwa ni watu ambao wamekuwa sehemu moja wamesoma shule moja na wamekuwa wakisaidiana kwenye mambo mbalimbali hata wakati Niva anafunga ndoa Nay alimsaidia kwa kiasi kukubwa.

 

Hata hivyo Niva ameweka wazi kuwa mambo hayo ya kudanganya mashabiki zao wameyaacha mwaka 2016 na mwaka huu hawatakuwa na mambo kama hayo kwa kuwa ni mwaka wa mafanikio zaidi kisanaa.

 

Niva na Nay wa Mitego walikuwa wanatupiana maneno machafu baada ya rapa huyo kumuimba Niva kwenye nyimbo ‘Shika Adabu Yako’ huku akimuita Supermario kitendo ambacho muigizaji huyo akupendezewa nacho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *