Muigizaji wa Bongo movie, Nisha amesema kuwa ujauzito wake unampa hisia tofauti na mawazo mpaka anafikia hatua ya kuposti mambo tofauti tofauti kwenye mitandao yake kwa kuwa hampendi mwanaume aliyempa ujauzito huo.

Nisha amesema amevumilia miezi mitano bila mtu kujua kitu chochote juu ya mimba yake lakini kwa sasa ameshindwa kuvumilia na hiyo ni kutokana na maumivu anayoyapata na kwamba mimba aliyoibeba ni ya mtu ambaye hampendi tena.

Pia Nisha amesema mwanaume aliyempa mimba ni mtu ambaye anapenda kujionesha sababu ambayo ilipelekea wakaachana.

Muigizaji huyo ameongeza kwa kusema kuwa anamuomba Mungu mtoto wake asifanane na baba yake na kama ikitokea akifanana naye hatakuwa anabudi ya kumficha bali atampa mtoto wake kila anachokitaka kwa kuwa mtoto hana kosa lolote.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *