Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Salma Jabu (Nisha) amesema kuwa mwaka huu atajikita zaidi kwenye kazi yake ya uigizaji kwa kuachia filamu baada ya kukaa kimya mwaka uliopita kutokana na kujikita katika biashara.

Nisha amesema kuwa mwaka uliopita alifanya filamu chache na kuutumia muda mwingi kwenye kujiimarisha zaidi katika biashara kuliko kutoa filamu mpya.

Baadhi ya biashara alizokuwa anafanya muigizaji huyo ni vipodozi pamoja na nguo ambapo ameamua kujikita huko kutokana na suala la kuigiza uwezi kufanya miaka yote hivyo ameonelea kuangalia masuala ya biashara.

Kupitia ukurasa wake Instagrama muigizaji huyo ameandika “Hakika 2016 ulikuwa ni mwaka wangu wa kufanya biashara tofauti na movie, 75% nimefanya biashara huku movie nikafanya 25% na yote hayo nilifanya ili kuweza kuweka msingi imara wa kujiingizia kipato bila kutumia ‘UNisha’ maana naimani kuna maisha baada ya haya na umri unasonga,”.

Pia ameongeza kwa kuandika “Mwaka mpya 2017 ni mwaka wa kuziba pengo la filamu nikiwa na Nishasfilmproduction. Ahsante Mungu aliye mwema kwenye biashara ndoto kubwa nliyokuwa naiwaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *