Muigizaji wa Bongo Movie, Salma Jabu ‘Nisha’ amewaonya watu wanaompiga vijembe msanii mwenzake, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa muigizaji, Steven Kanumba.

 Nisha aliiambia Full Shangwe kuwa, kwa kipindi kigumu alichonacho Lulu si cha kumnanga bali cha kumpa faraja.

“Tangu kesi ya Lulu ianze upya kusikilizwa, kuna watu wamekuwa wakimkashifu kwa maneno ya ajabu, bila kujua kuwa hakuna ajuaye ya kesho. Ni vyema tukampa faraja rafiki yetu kwa kipindi kigumu alichonacho,”.

Jana Mahakama kuu imemkuta na kesi ya kujibu muigizaji huyo baada ya kumuua bila kukusudia muigizaji wa Bongo Movie Steven Kanumba ambapo jana ameanza kujitetea.

Baada ya Lulu kuanza kujitetea amesimulia jinsi ilivyokuwa siku ya tukio, Lulu amesema marehemu alikuwa akimpiga na panga baada ya kutokea ugomvi uliotokana na wivu wa mapenzi, alipomuona akiongea na simu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *