Muigizaji wa Bongo movie, Salma Jabu ‘Nisha’ amesherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa aina yake baada ya kuamua kutembelea wagonjwa katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.

Nisha amesherehekea siku yake ya kuzaliwa tarehe 28 mwezi huu amesema maisha yake kwa sasa ameamu kuyaelekeza kwa kusaidia watu na siyo kutafuta skendo kama ilivyokuwa hapo awali.

Muigizaji ameendelea kwa kusema kwamba siku hizi anatumia muda mwingi kusaidia watoto yatima na wagonjwa kwa kuwa ameamua kuachana na skendo na hata watu anaokuwa nao mara nyingi ni watu ambao hawapendi skendo pia.

Kwa upande mwingine Nisha alitumia fursa hiyo kuwasaidia mahitaji yao ya matibabu na mahitaji madogo madogo ili mradi tu kuhakikisha anamalizia siku yake ya kuzaliwa na wagonjwa ambapo aliamua kujumuika nao katika siku hiyo.

Nisha ni muigizaji maarafu nchini Tanzania ambaye ameigizaji filamu tofauti zikiwemo Tikisa, Pusi na Paku pamoja na Betina na Zena.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *