Muigizaji wa Bongo Movie, Salma Jabu ‘Nisha’ anadaiwa kuwa kwenye mahusiano na aliyekuwa mpenzi wa msanii mwenzake Shilole anayejulikana kwa jina la Boy Caro.

Nisha anapika na kupakua na mwanaume huyo bila hata aibu ambapo amehama Mbezi Makonde jijini Dar alikokuwa akiishi mwanzo na kuhamia Mikocheni kwa mwanaume huyo.

Mapenzi ya Nisha na Boy Caro siyo siri tena kwani wanaishi pamoja, wanapika na kupakua hata hivi karibuni aliweka mtandaoni picha ya mkono wa mwanaume uliochorwa tatuu ambapo watu waligundua kuwa ni wa Boy Caro kwani aliichora wakati yupo na Shilole.

Kuhusu taarifa hizo zilizoenea katika mitandao ya kijamii, Nisha amesema kuwa kama ni Shilole walishaachana, ukaribu unaweza usiwe wa mapenzi, unaweza kuwa wa kikazi na mambo mengine, kuhamia Mikocheni siyo kwa ajili yake bali niliamua kubadilisha mazingira tu.

Taarifa za wawili hao kuwa katika mahusiano zimenea sana katika mitandao ya kijamii kutokana na ukaribu wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *