Video ya wimbo wa staa wa Bongo fleva, Vanessa Mdee ijulikanayo kama ‘Niroge’ imetajwa kuwania tuzo zinazoitwa ‘Loeries’ nchini Afrika Kusini.

Ni tuzo kubwa ambazo hushindanisha kazi mbalimbali za ubunifu kuanzia kwenye sekta zote za habari na mawasiliano katika Bara la Afrika.

Video hiyo ya Niroge imetajwa kuwania kipengele cha video bora ya muziki Barani Afrika.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Vanessa Mdee aliandika “Our #Niroge video has been nominated for a #Loerie2016 ( Google Them ) in the Music Video category. Later on today we will find out if we win this prestigious award,”.

Kwenye kipengele hicho video hiyo imeshindanishwa na video zingine kama , Everything ya M.I kutoka Nigeria, Jump ya Anatii, Cassper Nyovest na Nasty C.

Video hiyo ya ya Niroge imeongozwa na Director maarufu Afrika, Justin Campos.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *