Mwanahip hop kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili ametumia akaunt yake ya Instagram kuwachana wasanii wanaodai wanamuziki wa kundi hilo wanabebwa na baadhi ya media nchini kutokana na nyimbo zao.

Nikki wa Pili ameandika hayo baada ya wasanii kusema kuwa wanamuziki wa kundi hilo wanabebwa ambapo Nikki amekanusha vikali kuhusu skendo hiyo.

Baadhi ya wanamuziki wanaosema Weusi wanabebwa na media ni Young Killer alipoimba mstari uliosema ‘Watu wanasema Joh anabebwa’.

Kupitia akaunti yake hiyo Nikki wa Pili ameandika  “January mpaka sasa nimesharekodi zaidi ya nyimbo 10 @gnakowarawara amerekodi zaidi ya nyimbo 20 labda ndio sababu nakaribia kufikisha miaka 10 kwenye game…. hainabahati/wala kubebwa… fanya kazi..

nikki-2

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *