Mwanamuziki wa hip hop, Nikki wa pili ameishauri mamlaka zinazohusika kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo kilicho sababisha ajali ya wanafunzi pamoja na walimu mkoani Arusha.

Nikki ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache tangu kutokea kwa ajali hiyyo Mkoani arusha iliyopelekea  jumla ya watu 36 kufafariki wakiwamo walimu, wanafunzi na dereva wa shule ya Lucky Vicent Academy.

Kupitia akaunti yake ya Instagram ameandika “Lakini baada ya mazishi lazima uchunguzi ufanyike, kujuwa hali ya gari lenyewe ilikuwaje, maadili ya dereva, na hali ya usimamizi/ukaguzi wenyewe ulikuwaje….. na hii ichukuliwe kuweka udhibiti kwa watu wote walio chukuwa dhamana ya kulea watoto kwa maana ya shule…uthibiti, usimamizi….. haswa katika mazingira haya ya biashara”.

nikiii

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *