Baada ya Rais Magufuli kupokea ripoti kuhusu uchunguzi wa mchanga wa madini kwenye makontena, Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nikki wa Pili amempongeza Rais Magufuli kuhusu suala hiyo.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Nikki wa Pili amempongeza Rais kwa hatua hiyo ya kupambana na ufisadi akisisitiza kuwa vita ya kuvunja mfumo wa kifisadi ni hatari sana lakini Rais Magufuli amethubutu kufanya hivyo.

Nikki wa pili amesema kuwa “Watanzania wanao pewa dhamana, wasipo amuwa kuwa waadilifu, umaskini uta andika historia tukufu kwa wa Tz, alafu kuha uhusiano gani kati ya uwekezaji na ufisadi…. maana kila kasha, wizi mkubwa utamkuta mwekezaji na wakala wake wa kitanzania (wasomi, viongozi, wafanya biashara)…

Ameongeza kuwa kusema “Yani ni kama ule uchumi wa kikoloni manufaa nikwa makampuni ya nje na kitabaka cha watanzania wachache…… nimpongeze mkuu wa nchi kwa kuamuwa kupambana na ufisadi huu…

Pia amesema kuwa “Ila vita ya kuvunja mfumo wa kiuchumi wa kifisadi ni hatari.. kina lumumba, nkruma, sankara, huko chile, nikaragwa, Venezuela, haiti, iran…. viongozi hawakupona….. ni vita kuu… Mungu akusimamie”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *