Mkali wa hip hop Bongo, Nikki wa Pili amekiri  kuwa aliamua kuokoka na kumpokea yesu baada ya kufanikiwa kurudi shuleni  tena ikiwa ni baada kukaa mtaani akisubiri  matokeo ya awamu ya pili (Second Selection) ya ufaulu.

Nikki amesema tukio la kuamua kumpokea Yesu (Kuokoka) kulimfanya kuimarisha mahusiano yake na Mungu kutokana na maajabu aliyotendewa kwani hakuwa na pesa za kumuwezesha kwenda kusoma shule binafsi.

“Nilivyokuwaga kidato cha tatu nilisimama mbele ya watu na kuokoka yaani kumpokea Yesu na kumrudia Mungu…….offcoz nilifanya hivyo kwakuwa alinitendea maajabu ya kunitoa kitaa kupitia matokeo mnaita ‘second selection’ nilikuwa sina issue kitaa wala sikuwa na fedha kwenda private schoool”.

Rappa Nikki wa Pili kwa sasa anafahamika zaidi kama msanii msomi ambaye kwa sasa anadaiwa kuwa yupo shule kwa ajili ya ngazi ya Uzamifu (PhD)

Nikki kwa sasa ana ngoma mpya inayokwenda kwa jina la Kihasara ambapo anadai Sehemu kubwa ya wimbo huo inazungumzia maisha yake halisi aliyowahi kupitia.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *