Mwanamuziki wa hip hop nchini, Nikki Mbishi amesema kuwa meneja wa wasanii, Babu Tale ni jipu ambalo rais Magufuli pamoja na waziri wa Habari, Utamaduni Wasanii na Michezo, Nape Nnauye hawawezi kuliona mpaka serikali ya awamu ya tano itakapomaliza muda wake.

Nikki Mbishi amesema kuwa serikali itahakikisha haki za wazawa zinalindwa ipasavyo hivyo tayari ofisi yake imeanzisha zoezi maalum la kupima na kutoa vibali vya ardhi yote nchini ambayo imehakikiwa na wataalam ili kuwatambua wamiliki halali wa ardhi.

Nikki Mbishi amesema anatarajia kuachia wimbo wake mpya alioupa jina la ‘Babu Talent’ ambao mashairi yake yanaonekana kumgusa meneja wa kundi la Tip Top Connection na kudai kuwa meneja huyo ni jipu na halitaweza kutumbuliwa katika awamu ya tano ya Rais Magufuli.

Katika baadhi ya mistari ya wimbo huo inaonesha kuwa Babu Talent ndiyo chanzo cha baadhi ya wasanii kupotea kimuziki licha ya wasanii hao kuwa na uwezo wa kufanya vizuri kwenye muziki.

Hapo awali msanii mwengine wa hip hop, ROMA Mkatoliki aliwahi kumdisi meneja huyo kwenye wimbo wake ‘Kaa Tayari’ baada ya mstari mmoja unaosema meneja kaikana Tip Top kamganda Dangote.

Mstari huo umetokana na Babu Tale kuwa karibu na Diamond ambaye anajulikana pia kwa jina la Dangote huku akilisahahu kundi lake la Tip Top Connection ambapo kwasasa linawasanii wawili wanaofanya vizuri ambao ni Madee na Dogo Janja.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *