Baada ya wimbo wa Roma ‘Zimbabwe’ kufanya vizuri baada ya kuachiwa hivi karibu, mkali wa hip hop Bongo, Nikki  Mbishi amempongeza Roma kwa mafanikio ya wimbo huo.

Nikki amesema kuwa wimbo huo ndani ya siku mbili umepata viewers zaidi 450,000 katika mtandao wa YouTube ni ishara ya kufanya vizuri na ni mafanikio katika level ya muziki wa hip hop hususani Tanzania.

Mwanamuziki huyo kutokea pande za Ukonga amesema kuwa alipoona ngoma hiyo kwa mara ya kwanza alishawishika na ikabidi aidownload na kuanza kuusikiliza alishtuka kidogo na kuhisi mbona kama jamaa kuna kitu anataka kukisema.

Pia Nikki amesema wimbo huo haupo negative tu kwamba Roma anaipinga serikali kwani kamsifia Mh. Rais Dkt. Magufuli kwa kujenga bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga.

Wimbo huo ulitambulishwa wiki iliyopita na mke wake Roma kwenye media tofauti nchini kutokana na mwanamuziki huyo kusafiri kwenda Zimbabwe.

Katika wimbo huo Roma ameelezea tukio lake la kutekwa pamoja na masuala mengine ya kijamii katika sekta za siasa na jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *