Kundi la kigaidi la Boko Haram limetoa kanda ya video, wanayodai inaonyesha wasichana waliotekwa nyara katika eneo la Chibok miaka miwili iliyopita.

Video hiyo, inamuonyesha mwanamume mmoja aliyejifunika uso wake, akiwa amejihami kwa silaha, akizungumza na kundi la wanawake takriban 50.

Mmoja wa wanawake hao amejitambulisha kuwa, Madia na kusema kuwa anatoka Chibok.

Msichana huyo amesema wenzake kadhaa wamejeruhiwa vibaya kutokana na mashambulizi ya angani ya wanajeshi wa Nigeria.

Msichana huyo ametoa wito kwa serikali kuwaachilia wanachama wa Boko Haram, ili wasichana hao waachiliwe huru.

Inaonekana kuwa Boko Haram inatumia video hiyo kuwafanya raia wa Nigeria kuwahurumia wasichana hao, na kuilazimu serikali kutimiza matakwa yao.

Serikali ya Nigeria haijasema lolote kuhusiana na video hiyo hadi sasa lakini wazazi wa wasichana hao wanaiomba serikali iwaachie mateka wa kundi hilo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *