Wanamuziki wa Marekani ambao walikuwa wapenzi, Nicki Minaj na Meek Mill wameachana rasmi baada kutoka usaliti ndani ya uhusiano wao.

 Inadaiwa kuwa mkali Meek Mill ndiyo aliyemsaliti mpenzi wake baada ya kutoka kimapenzi na msichana ajulikanaye kama Sonye licha ya Meek Mill kukanusha madai hayo.

Wiki iliyopita mashabiki waligundua kuwa Meek na Nicki hawafatani tena kwenye mtandao wa kijamii wa instagram na jambo hili limechochea taarifa za kutengana kwao.

Meek Mill aliweka picha instagram iliyoambatana na ujumbe “$avage…just friends.” ila mpaka sasa haijajulikana mwanamke huyu ni nani.

Meek Mill na Nicki Minaj wamekuwa kwenye uhusiano toka February 2015 baada ya hapo walikuwa wanaambatana kila sehemu tofauti na ilivyosasa.

Kwa mujibu wa Gossip kuwa Sonya ni mmiliki wa duka la nguo na amekuwa na Meek kwa zaidi ya mwka mmoja huku Meek akiwa kwenye mahusiano na Nicki Minaj.

Nicki Minaj na Meek Mill kwa sasa wanaishi nyumba tofauti huku kambi ya Nicki Minaj ikithibitisha kuwa hawako pamoja kwenye mahusiano.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *