Rapa wa kike na supastaa wa Marekani, Nicki Minaji na mwenzake Ariana Grande wamejumuishwa kwenye orodha ya mastaa watakaofanya shoo kwenye utoaji wa tuzo za MTV VMA utakaofanyika mwishoni mwa wiki hii.

Mastaa hao wanatarajia kupanda jukwaa moja na kufanya shoo kwa pamoja kwenye ukumbi maarufu wa Madison Square Garden siku ya Jumapili.

Pia staa mwengine anayetarajia kufanya shoo siku hiyo niBritney Spears ambaye atakuwa amerejea kwa mara nyingine kwenye kufanya shoo kwenye MTV VMA tangu alipofanya hivyo mikama 9 iliyopita.

Nick Jonas na Rihanna ambaye atapewa tuzo kubwa kabisa kwenye usiku huyo ya Michael Jackson Video Vanguard Award pia watafanya onyesho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *