Mwanamuziki nyota wa Marekani, Nicki Minaj amemdis mpenzi wake zamani Meek Mill kwenye shiw yake mjini Paris nchini Ufaransa.

Minaj ambaye kwa sasa yupo kwenye beef kubwa na Remy Ma ametumia sekunde chache kwenye show yake na Drake kumdiss Ex Wake huyo.

Wakati wanafanya show yao Minaj na Drake waliimba nyimbo kama “Moment 4 Life,” “Truffle Butter,” na diss yake kwa Remy Ma, “No Frauds.”

Katikati ya show hio Minaj alizima mziki nakusema “Nawashauri mkimbize ndoto zenu na msikubali kutoka kwenye njia zenu, nyie ni muhimu, na kama mwanaume hajui jinsi ya kukujali vizuri, anabidi atoke kwenye maisha yako’.

Wawili hao walikuwa wapenzi kwa miaka miwili lakini kwasasa wameachana kutokana na kutoelewana baina yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *