Mwanamuziki wa Marekani, Nicki Minaj ameahidi kulipa karo za shule kwa baadhi ya wanafunzi ambao ni mashabiki wake.

Nicki Minaj  amesema ni lazima wathibitishe kwamba walipata alama A katika mtihani wao wa kujiunga na vyuo.

Alikuwa akijibu maombi kutoka kwa mashabiki wake kwenye Twitter ambao walitaka awape pesa.

Baada yake kusema atasaidia wale waliopata alama A, baadhi walimtumia kwenye Twitter picha za matokeo yao ya mtihani na kumweleza matatizo ya kifedha yanayowakabili.

Wengi walikuwa wanaomba msaada wa chini ya $1,000 (£770) lakini katika kisa kimoja, alionekana kuwa tayari kutoa msaada wa $6,000 (£4600) kwa mwanafunzi mmoja, iwapo angethibitisha anataka kuzitumia wka njia gani.WITTER

Mwanamuziki huyo amejitolea kuwasaidia mashabiki 30 ambao walimuonesha vyeti vya matokeo lakini wameshindwa kujilipia karo za shule.

Mapema mwana huu, mwanamuziki huyo alitoa $1m (£870,00) zakusaidia shule mjini Chicago.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *