Staa wa Bongo Movie na mshindi wa kimataifa wa tuzo ya filamu bora, Elizabeth Michael a.k.a Lulu ametangaza ujio wa kazi yake mpya, NI NOMA ambayo inatarajia kuzinduliwa rasmi siku ya kesho jijini Dar es Salaam.

Filamu hiyo ambayo inatarajia kuja na mabadiliko kwenye tasnia ya filamu hapa Bongo hususani baada ya Lulu kujifunza vitu kadhaa alipokwenda kupokea tuzo ya ushindi nchini Nigeria inatarajia kuanza kuuzwa kwa njia ya mtandaoni kupitia application ya Proin Box.

Ushindi: Lulu akifurahia tuzo ya AMVCA
Ushindi: Lulu akifurahia tuzo ya AMVCA

lulu1

‘Mashabiki wetu watafurahi zaidi kwasababu tumerahisisha njia za kuiuza filamu hii ambapo fans watanunulia mtandaoni kupitia huduma za mobile money’.

Pia, filamu hiyo inatarajia kuingizwa kwenye majumba ya sinema na kisha kuanza kuuzwa kwa njia ya DVD ambazo zitakuwa na nyongeza ya video za behind the scenes, interviews za wahusika mbalimbali na vitu vingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *