Hakuna kitu ambacho kinapofanywa bila fikra yakinifu basi huleta faida pasipo kuleta hasara.
Kwa wasanii wengi wa Tanzania hususani kwa zama hizi, maisha yamebadilika sana, hakuna tena jambo la siri kwenye maisha yao. Kila kitu HADHARANI. Mambo ya sebuleni, uani, chumbani, jikoni na popote pale, ukiingia kwenye mitandao ya kijamii utayakuta.

Linah

Mtu akimtendea jambo jema mzazi wake, atatangaza…..’Leo nimemnunulia mzazi wangu nyumba/gari, hapa nikiwa na kampani yangu tukimkabidhi mzazi wangu funguo za mali yake mpya. Mzazi mzaa chema huyooo, Mzazi wa mieee, mzazi ya mutu mukubwa………na maneno mengine chungu mzima.

Athari za mambo kama haya huwa hazijitokezi kwa haraka lakini pindi mambo yanapobadilika kidogo tu… yanarudi tena KULE KULE YALIKOANZIA (mtanadoni) lakini yakiwa na sura ya kusikitisha, kukarahisha na kufedhehesha.

Utakuta maneno ya kebehi na dharau anaulizwa staa wa Tanzania ambaye aliwahi kuonyesha ufahari mtandaoni: ‘Ile nyumba/gari imekuwa daladala/gesti siku hizi maana naona watumiaji tumekuwa wengi…….mzazi wa mutu mukubwa

‘KAPOKKONYWA TENA? Au ndio ilikuwa ‘NIPISHE NIPIGE SELFIE nikawarushe roho mtandaoni? Na mbaya zaidi panaambatanishwa picha za wahusika na kitu kinachozungumziwa na ikiwezekana na picha za ulinganisho wa mambo yalivyokuwa na mambo yalivyo…….FEDHEHA KUBWA KWAKWELI.
Ukitaka kuyajua zaidi hayo basi muulize staa wa OLE THEMBA…..Linah Sanga. Juzi alipokuwa anafanyiwa mahojiano na mtandao wa Bongo5 alikiri kuwa kosa alilolifanya kwenye maisha yake ya kikazi ni kuanza kuyaweka wazi mahusiano yake ya kimapenzi.

Linah ameshuka kimuziki katika tafsiri kuwa, uwezo wa kuimba na kutunga bado anao lakini mashabiki hawafuatilii tena kazi zake za kimuziki, wanafuatilia kujua maisha aliyowaonjesha yanaendeleaje?
Je, wasanii wangapi wako kwenye mstari wa kuelekea kupotea namna hiyo?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *