Unadhani ni nyimbo gani ambayo imechukua muda mrefu zaidi kuandikwa kwenye Bongo Fleva?

Bado IshiKistaa inafanya utafiti huo lakini maneno ya hivi karibuni ya staa wa zamani wa THT, Pipi kuwa ngoma yake HAFAI aliyomshirikisha Nikki wa Pilli imechukua miaka mitatu kuiandika huenda ikawa ndio ngoma inayoshikilia rekodi ya kuchukua muda mrefu zaidi kuandikwa.

Pipi baada ya kuwika sana akiwa na THT alipotea kidogo kwenye muziki kutokana na majukumu mengine ya kimasiha kumhitaji na sasa amerudi tena kuwakumbusha fans wake kuwa she is still a top singer.

Je, maudhui ya ngoma HAFAI yanaweza kuufanya wimbo huop kudumu kwenye chati za Bongo Fleva kwa muda mrefu kama ambavyo ulivyomgharimu muandishi wake muda mrefu?

Ni wasaa wa kusubiri ni kuona kitakachojiri na kuamuliwa na fans wa Bongo Fleva kwenye ngoma hiyo ingwa Pipi mwenyewe anakiri kuwa ushindani kwenye soko la Bongo Fleva umeimarika vya kutosha kiasi ambacho ngoma ya msanii kudumu kwenye chati za juu za Bongo Fleva kwa zaidi ya miezi 12 si jambo dogo.

MUHIMU:

Hii ni nafasi ya mashabiki wa IshiKistaa kututajia ngoma ambayo wasanii wake walidai kuwa waliiandika kwa muda mrefu zaidi nasi tutakamilisha utafiti wetu kisha kuwazawadia fans watakaopatia.

Comment kwenye Facebook page yetu, Instagram na Twitter.

Swali:

Ni ngoma gani ya Bongo Fleva ambayo iliandikwa kwa muda mrefu zaidi?

https://www.facebook.com/ishikistaa/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *