Mshambuliaji wa Yanga SC, Donald Ngoma, raia wa Zimbabwe anaweza kuikosa mechi dhidi ya Simba Oktoba 28.

Hii inatokana na kuandamwa na majeraha mfululizo, hivyo umechukua uamuzi wa kumpumzisha kwa siku saba kuanzia jana kutokana na kuonekana majeraha yake hayajapona vizuri.

Afisa Habari wa Klabu hiyo, Dismas Ten amesema, Ngoma amepewa siku saba za mapumziko kwa ajili ya kuangalia afya yake huku akiwa anaendelea na matibabu ili kuimarika kwa ajili ya kurejea akiwa salama kwenye mapambano ya ligi.

Ngoma alianza kuumwa misuli ya paja hivi karibuni ambapo amelazimika kupewa siku saba kwa ajili ya mapumziko ili kuangalia  afya yake kabla ya kuanza mazoezi mepesi.

Timu ya yanga inatarajia kusafiri leo au kesho kwenda Bukoba kuivaa Kagera Sugar, mechi hiyo ya Jumamosi sasa ni uhakika Ngoma ataikosa.

Yanga na Simba zitavaana katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara Oktoba 28 mwaka huu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *