Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma amekanusha tetesi za kujiunga na klabu ya Simba baada ya mkataba wake kumalizika.

Ngoma amekanusha tetesi hizo baada ya kuenea uvumi kwenye mitandao kuwa anataka kujiunga na Simba baada kutoonekana katika kikosi cha timu hiyo.

Mshambuliaji huyo amesema kuwa kuwapo kwake nje kumetokana na kuumia kwake lakini si kwamba anataka kuihama timu hiyo.

Ngoma amesema kuwa uongozi wa klabu hiyo umempa ruhusa ya kupumzika na hajatoloka kwenda Afrika Kusini kutafuta timu zaidi ya kufuata matibabu ya kisasa nchini humo.

Mshambuliaji ameongeza kwa kusema kuwa hadi sasa hajasaini mkataba mpya na klabu hiyo pamoja na kuwa tayari kufanya hivyo endapo watakubaliana na masharti yake.

 

Ngoma hajaichezea klabu yake ya Yanga toka mwezi Januari mwaka huu kutokana kusumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *