Baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu hatimaye mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma amerejea kikosini kwaajili ya maandalizi ya kuivaa Singida United kwenye mchezo wa kombe la shirikisho (ASFC).

Ngoma alipata majeraha ya goti katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar, mchezo uliopigwa Septemba 30, mwaka jana ambapo majeraha hayo yamemuweka nje ya uwanja kwa miezi sita.

Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga, Hussein Nyika amesema kwamba kwa mujibu wa taarifa za daktari wa timu hiyo nyota huyo yupo fiti kuanza mazoezi.

Aidha Nyika amesema wachezaji wote waliokuwa majeruhi wamepona na kuungana na kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo wa kombe la ASFC utakaopigwa April 1.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *