Kiungo wa Chelsea, N’golo Kante ameshinda tuzo ya PFA ya mchezaji bora wa mwaka wa Uingereza baada ya kuwashinda Eden Hazard, Harry Kane, Romelu Lukaku, Zlatan Ibrahimovic na Alexis Sanchez.

Dele Alli wa Tottenham ameshinda tuzo ya mchezaji bora mdogo wa PFA wakati Lucy Bronze wa Man City ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa kike.

 Mchezaji wa zamani wa Manchester United, David Beckham ameshinda tuzo ya heshima kwa mchango wake katika soka.

N’golo Kante alikuwa mchezaji muhimu na kuisadia Leicester City kutwaa Ubingwa wa EPL msimu uliyopita na sasa yupo Chelsea iliyopo katika mbio za Ubingwa.

Kama atafanikiwa kutwaa taji la EPL atakuwa mchezaji wa kwanza kuwahi kufanya hivyo mara mbili mfululizo akiwa na timu mbili tofauti.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *