Aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini, katika serikali ya awamu ya nne, William Ngeleja amesema kuwa muda mrefu Serikali ilikuwa na mpango wa kutengeneza mtambo wa kuchenjua madini.

Amesema hayo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akifafanua tuhuma zinazotolewa kwa viongozi wa wizara hiyo  waliokuwepo wakati mikataba ya madini inasainiwa kwamba hawakufanya chochote wizi na udanganyifu unaendelea kwenye sekta ya madini.

Kauli hiyo ya Ngeleja ambaye ni mbunge wa Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza imekuja kufuatia kukiwa na malalamiko kuwa viongozi waliopita katika wizara hiyo hawakuchukua hatua kuhakikisha suala la kusafirisha mchanga wa madini linafanyiwa kazi.

Wiki chache zilizopita Rais Magufuli alimfuta kazi waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo baada ya kushindwa kufanikisha mchanga wa dhahabu kutosafirishwa kwenda nje ya nchi.

Kwa upande wake waziri mkuu, Kassim Majaliwa aliwaoa hofu wawekezaji wa madini nchini kusubili ripoti ya pili kuhusu mchanga huo wa madini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *