Kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Ngassa amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na klabu ya Fanja ya nchini Oman.

Ngassa aliyesaini baada ya mazungumzo na Mwenyekiti wa klabu, Sheikh Saif Abdullah Al-Sumri mwishoni mwa wiki amesema kwamba anafungua ukurasa mpya wa maisha yake ya soka.

 Ngassa anajiunga na wawakilishi hao wa Oman kwenye Ligi ya Mabingwa ya Asia, kiasi cha wiki tatu tangu avunje mkataba na klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini.

Ngassa: Akikabidhiwa fomu yake baada ya kusaini mkataba na timu ya Fanja ya Oman.
Ngassa: Akikabidhiwa fomu yake baada ya kusaini mkataba na timu ya Fanja ya Oman.

Ngassa alijiunga na Free State Stars Mei mwaka jana akisajiliwa na kocha Mmalawi, Kinnah Phiri kwa mkataba wa miaka minne.

Ngassa pia aliwahi kuzichezea timu za Toto Africans ya Mwanza, Kagera Sugar ya Bukoba, Yanga SC, Azam FC na Simba za Dar es Salaam kabla ajaelekea nchini Afrika Kusini na sasa kasaini Fanja ya Oman.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *