Winga wa zamani wa Taifa stars, Mrisho Ngassa amevunja mkataba na timu ya Free State Stars ya Afrika kusini baada ya pande zote mbili kufikia makubaliano ya kuvunjika kwa mkataba huo.

Ngassa ambaye pia alizichezea klabu za Yanga, Simba na Azam FC alijiunga na klabu hiyo Mei mwaka jana  ambapo alisajiliwa na kocha Kinnar Phiri na kudondosha wino wa miaka minne kwa sasa mchezaji huyo yupo huru kujiunga na timu yoyote.

Klabu ya Free State Stars FC ya Afrika Kusini ilitoa barua ya kuvunjwa mkataba huo na Meneja Mkuu Rantsi Mokena inaonesha mkataba huo umevunjwa tangu Agosti 25 mwaka huu.

Kutokana  na kuvunjika kwa mkataba huo Ngasa kwasasa hana timu kwa maana ni mchezaji huru na anaweza kwenda na kujinga na timu yoyote itakayohitaji huduma ya mchezaji huyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ngasa amesema anamshukuru Mungu kuvunjika kwa mkataba huo na yupo huru kwasasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *