Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar amewasili nchini Ureno kwaajili ya kufanyiwa vipimo vya afya kujiunga na klabu ya PSG kwa ada ya pauni milioni 198.

Dau hilo la Neyma linamfanya kuweka rekodi ya dunia akitokea Barcelona baada ya makubaliano.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazili amewasili Ureno jana usiku baada ya kuuwambia uongozi wa Barca kuwa anahitaji kuondoka na kujiunga na PSG kwa dili ambalo litamuhakikishia kulipwa pauni 500,000 kwa wiki.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, hakufanya mazoezi na Barcelona siku ya Jumatano na amepatiwa ruksa ya kuondoka katika klabu hiyo.

Mtandao wa Barcelona umetoa maelezo kuwa “Neymar Jr, akiwa na Baba yake na wakala wake wamethibitisha kuondoka kwa mchezaji huyo baada ya kukaa kikao na ofisi za klabu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *