Baada ya kuomba kuhama katika klabu ya Barcelona, Neymar amesema kuwa anahitaji changamoto mpya ndiyo mana ameamua kuhamia Paris Saint Germain ya Ufaransa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alishinda mataji saba muhimu katika misimu yake minne katika uwanja wa akiwa na Barcelona ikiwemo taji la klabu bingwa mara moja na lile la La Liga mara mbili.

Neymar amesema kuwa ameshinda mataji yote aliyokuwa anahitaji akiwa na Barcelona tok ajiunge akitokea Santos ya kwa Brazil.

Uhamisho wa Neymar umevunja rekodi ya awali iliowekwa na Paul Pogba aliporudi kuichezea Manchester United kutoka Juventus kwa kitita cha £89m mnamo mwezi Agosti mwaka huu.

Mshahara wake wa £782,000- kwa wiki unamaanishi kuwa PSG itamlipa Paundi muilioni 400 kwa wiki.

Neymar anatarajiwa kutangazwa mbele ya mashabiki wa PSG katika uwanja wa Parc des Princes jijini Paris kesho Jumamosi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *