Mshambuliaji wa Barcelona, Neymar Jr ameipatia klabu yake ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Manchester United kwenye mechi ya fainali ya michuano ya International Champions Cup iliyofanyika nchini Marekani.

Neymar aliipatia goli klabu yake ya Barcelona katika dakika ya 31 ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo ambao ulikuwa unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka duniani.

Kwa matokeo hayo Barcelona wametwaa taji la michuano hiyo ambalo lilifanyika nchini Marekani.

Mchezo mwingine uliopigwa ni kati ya Juventus na PSG ambapo mabingwa hao wa Italia wameshinda 3-2.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *