Aliyekuwa mshiriki wa mashindano ya Miss Tanzania mwaka 2008, Nelly Kamwelu amekiri kudanganya umri katika mashindano hayo wakati huo ili apate fursa ya kushiriki.

Mrembo huyo amesema kuwa wakati huo umri wake ulikuwa ni miaka 15, lakini ilibidi ajikuze ili kukidhi vigezo na kuamua kuandika umri wa miaka 18.

Pia amesema sababu kubwa ya kulazimisha kushiriki katika mashindano hayo ni ndoto aliyokuwa nayo tangu akiwa mdogo lakini umbile lake lilikuwa linamruhuruhusu kwa kuwa alionekana kuwa na mwili mkubwa licha ya kuwa na umri mdogo.

Ukweli huo unaonesha jinsi ambavyo ni rahisi kwa warembo kudanganya umri wao katika mashindano hayo, pasipo kugundulika

Nelly mbali na kushiriki mashindano hayo ya Miss Tanzania ambayo hakuambulia kitu amesema hakukata tamaa na hivyo kuingia katika mashindano mengine ya urembo ambayo yalikuwa ni Miss Universe Tanzania mwaka 2011 na kuibuka mshindi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *