Mwanamuziki wa Marekani, Nelly amefunguka jinsi ambavyo anajipanga kuanika kila kitu kuhusu kukamatwa kwa tuhuma za kumbaka mwanamke ndani ya gari.

Katika madai hayo, Mwanamke huyo ameeleza kuwa timu ya Nelly ilimualika kwenye hafla yao na kisha akaondoka na gari na watu wa rapa huyo ambao walimuhamishia kwenye gari lake (Nelly).

Amesema akiwa kwenye gari hilo, Nelly alimlazimisha kufanya naye mapenzi tena bila kutumia kinga, kitu ambacho msichana huyo alikipinga.

Hata hivyo, anadai Nelly alimlazimisha na kumtaka ‘kufunga mdomo wake’ na kisha akatekeleza matakwa yake bila kinga.

Mwanamke huyo ameeleza kuwa baada ya kumfanyia kitendo hicho, Nelly alimpa fedha lakini alikataa.

Anasema Nelly alimfukuza kwenye gari lake na kumrushia kitita cha fedha kiasi cha dola za kimarekani 100 ($100).

Timu ya Nelly imekanusha vikali tuhuma hizo na kueleza kuwa imejipanga kuuanika uongo wake.

Mwanasheria wa Nelly, Scott Rosenblum amesema kambi yao imemuajiri mpelelezi binafsi ambaye atafuatilia na kuweka wazi kilichofanyika katika tukio hilo, kwa kutumia teknolojia.

Rosenblum amesema kuwa mwanamke huyo anajitahidi kutafuta umaarufu na fedha kupitia uongo ambao ameupika kama mwandishi wa vitabu vya kutunga.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *