Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC), Ramadhani Kailima ametoa ufafanuzi juu ya matokeo ya uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani Zanzibar uliofanyika Januari 22 mwaka huu.

Kailima amesema kuwa wapiga kura walioandikishwa katika jimbo la Dimani, Zanzibar walikuwa 9,275 kwa wapiga kura wote.

Kati ya hao waliopiga Kura walikuwa 6,406, Kura halali 6,172 na Kura zilizoharibika zilikuwa ni 234 kwenye uchaguzi huo.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa vyama 11 vilishiriki kwenye uchaguzi huo ambapo chama cha ACT – Wazalendo kura nane Chama cha ADC kura 42, Chama Cha Mapinduzi kura 4860, Chauma kura 10, Chama Cha Wananchi (CUF) kura 1234 na Chama Cha DP kura 8.

Uchaguzi huo mdogo wa Jimbo la Dimani umefanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Hafidh Ali Tahir (CCM) kilichotokea Novemba 11 mkoani Dodoma alikokuwa akihudhuria Mkutano wa Bunge na kuugua ghafla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *