Spika wa Bunge Job Ndugai amefanya mabadiliko ya Wajumbe wote Ishirini na nne (24) wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI k wa kuunda upya kamati hiyo na kuteua wajumbe Wapya Kumi na sita (16) amba o pia watakuwa ni wajumbe katika kamati nyingine za Kudumu za Bunge.

Taarifa ya Ofisi ya Bunge mjini Dodoma imesema mabadiliko hayo yamelenga kuwawezesha wabunge kujifunza na kujipatia uelewa na uzoefu zaidi katika kutekeleza shughuli mbalimbali za Kamati za Bunge ambapo wabunge wote waliokuwa wajumbe wa Kamati ya Masuala ya UKIMWI hapo awali, wamepangiwa Kamati zingine kwa nia ya kuboresha utekelezaji wa majukumu ya kibunge.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo msingi wa mabadiliko haya unatokana na Ibara ya 96 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inayolipa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mamlaka ya kuunda Kamati za Bunge za namna mbalimbali kadri linavyoona inafaa kwa ajili ya kurahisis ha utekelezaji wa majukumu yake na Kanuni ya 116 (3) – (5) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016 inampa Spika Mamlaka ya kuteua Wabunge ili wawe Wajumbe katika Kamati mbalimbali za Bunge ikiwa ni pamoja na Mamlaka ya kuongeza, kubadilisha au hata kupunguza idadi ya Wajumbe katika Kamati za Kudumu za Bunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *