Zaidi ya watu 32 wamefariki dunia baada ya ndege ya kubeba mizigo ya Uturuki iliyokuwa safarini kutoka Hong Kong kuangukia nyumba za watu karibu na mji wa Bishkek nchini Kyrgyzstan.

Ndege hiyo aina ya Boeing 747 ilianguka karibu na uwanja wa ndege wa Manas, takriban kilomita 25 kutoka mji mkuu Bishkek, serikali ya Kyrgyzstan imesema.

Nyumba zaidi ya 15 zimeharibiwa na watoto kadha wanaripotiwa kuwa miongoni mwa waliofariki.

Ndege hiyo ilikuwa imepangiwa kutua kwa muda Manas na kisha kuendelea na safari hadi Istanbul, uturuki.

Ndege hiyo inamilikiwa na shirika la ndege za kubeba mizigo la ACT, ambayo hujitambulisha kama MyCargo.

Hata hivyo, serikali ya Kyrgyzstan inasema ndege hiyo ilikuwa inasafiri chini ya shirika la ndege la serikali ya Uturuki,

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *