Ndege itakayowabeba wanafunzi majeruhi waliopata ajali wilayani Karatu mkoani Arusha inatarajia kuwasili leo nchini.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu wakati akiwa katika hospitali ya mkoa wa Arusha Mount Meru ambapo wanafunzi wamelazwa.

Nyalandu amesema kuwa wamekamilisha  safari ya kuwapeleka Marekani majeruhi watatu wa ajali iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa Shule ya Lucky Vincent ya Arusha.

Akizungumza katika ofisi ya mganga mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru jana Nyalandu amesema ndege maalumu ya kuwabeba majeruhi hao  imetolewa na Shirika la Samaritan Fund la nchini Marekani ambayo itawasili kesho.

Nyalandu amesema rubani anatarajiwa kuwasili jijini Arusha leo akitokea Nairobi nchini Kenya na iwapo kila kitu kitakamilika safari itakuwa Jumamosi.

Nyalande ambaye alikuwa waziri wa Utalii na Maliasili katika Serikali ya awamu ya nne amesema kuwa watakaondoka ni abiria wanane ambao ni majeruhi wenyewe na wazazi waki muuguzi mmoja na daktari mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *