Ndege ya shirika la ndege la Malawi inayoongozwa na wanawake watupu imefanikiwa kutua salama jijini Dar es Salaam nchini Tanzania leo.

 Shirika hilo limefanikiwa kukamilisha safari ya ndege iliyosimamiwa na wanawake pekee ambapo imetua katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam.

Marubani na wasaidizi wa abiria kwenye ndege hiyo wote walikuwa wanawake na ni mara ya kwanza kwa shirika hilo kuandaa safari kama hiyo.

Ndege hiyo ilianza safari yake mjini Blantyre na ikatua kwa muda Lilongwe kabla ya kuelekea Dar es Salaam.

Ndege hiyo ilikuwa chini ya Kapteni Yolanda Kaunda akisaidiwa na Lusekelo Mwenifumbo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *