Mastaa wengi wa Bongo Movie walianza kuonekana baada ya kupata msaada wa mastaa waliowakuta kwenye game wakati huo.

Hata hayati Kanumba aliwakuta kina marehemu Mzee Jongo, Mzee Pwagu na wengine kwenye game kisha nao wakampa maarifa na ufundi na alipoongeza na jitihada zake na kipaji chake nae akawa staa anayekumbukwa hadi leo hapa nchini.

Hali ya kusaidiana miongoni mwa wasanii imeendelea kwa miakammingi kuwa uti wa mgongo wa kukua na kuendelea kuwepo kwa sanaa ya Bongo Movie huku mmoja wa mastaa ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika kukuza vipaji vya mastaa wachanga akiwa ni Rose Ndauka.

Kwa kupitia kampuni yake, Rose amekuwa akipambana kuwapa nafasi wasanii chipukizi ili waweze kuthibitisha vipaji vyao.

Staa huyo anataka kuja na tamthiliya yake iitwayo ‘How Cheat?’.

Ili kuifanikisha tamthiliya hiyo, staa huyo ametoa fursa kwa wasanii chipukizi kuonyesha vipaji vyao.

Je, una kipaji cha kuigiza? Unamfahamu mwenye kipaji cha kuigiza? Fursa ndio hii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *