Nchi za kiarabu za Saudi Arabia, Misri, Bahrain, Milki ya nchi za kiarabu na Yemen wamekata uhusiano wao wa kidiplomasia na Qatar wakiilaumu wa kuvuruga eneo hilo.

Nchi hizo zimeilaumu Qatar kwa kuunga mkono ugaidi likiwemo kundi la Muslim Brotherhood.

Shirika moja nchini Saudi Arabia linasema kwa limefunga mipaka yake na kusitisha usafiri wa ardhini baharini na angani.

Lilinukuu maafisa wakisema kuwa hatua hiyo ni ya kulinda usalama wa nchi kutokana na hatari za ugaidi na itikadi kali.

Kile ambacho kwa wiki kadhaa kimekuwa kikichochea mzozo baina ya mataifa ya Ghuba sasa kimelipuka kuwa mzozo kamili wa kidiplomasia .

Katika tangazo la pamoja , Saudi Arabia ilikuwa ya kwanza kusema kuwa inavunja mahusiano yake ya Qatar mapema Jumatatu , mara moja ikafuatiwa na Bahrain, Muungano wa Milki za kiarabu Misri na Yemen.

Hatua za kwanza za mzozo huu zilionekana kujitokeza mwezi Mei wakati Qatar iliposema shirika lake rasmi la habari lilidukuliwa pamoja na kauli ambayo haikuwa sahihi iliyosemekana kutolewa na mtawala wake, iliyoonekana kwenye mtandao ikisifu kundi la wanawamgambo wa Iran na Lebanon la Hezbollah.

Misri nayo imefunga anga zake na bandari kwa Qatar, kwa mujibu wa wizara ya mashauri ya nchi kigeni.,

Milki ya nchi za kiarabu imewapa wanadiplomasia wa Qatar saa 48 kuondoka nchini humo huku Abu Dhabi inaishutumu Qatar kwa kufadhili ugaidi na itikadi kali.

Shirila la taifa la habari nchini Bahrain nalo limesema kuwa nchi hiyo inataka uhusiano na Qatar kwa kuvuruga usalama wake na kuingilia ndani masuala yake ya ndani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *