Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwingulu Nchemba leo ameongoza waombolezaji waliojitokeza kuaga miili ya askari nane waliouawa wilayani Kibiti mkoani Pwani.

Akizungumza wakati wa kuaga miili hiyo, Nchemba amesema kuwa atahakikisha watuhumiwa wote waliohusika kufanya tukio hilo wanapatikana na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akitoa pole kwa wafiwa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akitoa pole kwa wafiwa.

Waziri huyo amewaomba wakazi wa Kibiti kutoa ushirikiano na Jeshi la Polisi ili kukabiliana na uhalifu wilayani humo.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchi, IGP Ernest Mangu amesema kuwa watuhumiwa wote waliofanya tukio hilo lazima watafutwe ili kokomesha vitendo hivyo ndani nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *