Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) imepitisha na kutangaza matokeo ya watahiniwa 6,282 waliofanya mtihani kati ya Novemba mosi hadi 4 mwaka huu katika ngazi mbalimbali za masomo, huku watahiniwa 2,898 wakishindwa kabisa katika mitihani yao.

Katika matokeo hayo, watahiniwa waliokuwa wamejisajili kufanya mitihani ni 6,917 ambapo kati yao watahiniwa 653 (asilimia 9.2), hawakufanya mitihani hiyo kutokana na sababu mbalimbali.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, Pius Maneno, ilieleza kuwa matokeo hayo yanafuatia mitihani iliyofanyika katika vituo 11 vya mitihani kutoka mikoa kadhaa ya Tanzania Bara na Visiwani.

Mitihani hiyo ilihusisha watahiniwa katika hatua ya kwanza na ya pili katika ngazi ya cheti cha utunzaji wa Hesabu (ATEC I, ATEC II) zenye masomo manne kila moja na ngazi ya taaluma, Hatua ya awali/msingi yenye masomo matano, Hatua ya Kati yenye masomo sita na hatua ya mwisho yenye masomo manne.

Taarifa hiyo ilibainisha kuwa watahiniwa 263, kati ya 6,282, waliofanya mitihani hiyo, wamefaulu huku wengine 281 (4.4%) wakifaulu katika mitihani yao waliyokuwa wameshindwa awali. Pamoja na ufaulu huo, watahiniwa 2,119 wameshindwa katika baadhi ya masomo yao huku 2,898 wakishindwa mitihani yao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *