Staa wa Hip-Hop nchini, Nay wa Mitego amesema kwamba amemalizana na Baraza la Sanaa nchini (BASATA) baada ya kutangaza kumfungia asijihusishe na masuala ya muziki kutokana na kuimba nyimbo zisizokuwa na maadili katika jamii.

Nay amesema amefanya marekebisho ya wimbo “Pale Kati” kama alivyoelekezwa na Baraza hilo na kwamba kuna version nyingine ya wimbo huo ambapo mojawapo itaruhusiwa kuchezwa kwenye media mbali mbali nchini.

Vile vile staa huyo amesema video nazo tayari zimeshafanyiwa marekebisho kama BASATA walivyotaka hivyo zitaanza kuoneshwa pindi zitakapokamilika.

Nay amesema kwa kifupi yeye na BASATA wameshamalizana kwasababu vitu walivyokuwa wanahitaji ameshavirekebisha na amewataka mashabiki wake kuwa tayari kwa kuipokea nyimbo hiyo baada ya kufanyiwa marekebisho.

BASATA walitangaza kumfungia Nay wa Mitego wiki iliyopita kutokana na nyimbo zake kukosa maadili katika jamii na zinalenga kuwadhalilisha sana wanawake. Nyimbo za Nay zilizowahi kufungiwa na BASATA ni “Shika Adabu Yako” na “Pale Kati”.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *